Story by Our Correspondents –
Zaidi ya familia 360,696 zilizoathirika na kiangazi kikali kote nchini zinatarajiwa kupokea shilingi elfu tatu kila mwezi ili kukidhi mahitaji yao hadi pale hali itakaporudi kuwa sawa.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuzindua rasmi mpango huo ambao unalenga kaunti 23 kote nchini, Waziri wa mipango maalum nchini Prof. Margaret Kobia amesema fedha hizo zitatumwa kwa wananchi hao kupitia njia ya Mpesa.
Waziri Kobia amedokeza kwamba tayari shilingi bilioni 6 zimetengwa kufanikisha mpango huo huku akiweka wazi kwamba zaidi ya mifugo elfu 76 watachukuliwa na serikali na kuchinjwa kisha kusambaziwa wakaazi walioathirika na ukame katika kaunti hizo 23.
Hatua hiyo imejiri baada ya serikali kutangaza kwamba ukame ni janga la kitaifa na linahitaji kushuhulikiwa kwa haraka ili kuzuia idadi kubwa ya wananchi kuathirika.