Picha kwa Hisani –
Serikali imetangaza kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 31 mwezi huu, itakuwa siku ya kitaifa ya mapumziko kwa ajili ya kuwawezesha Waumini wa dini ya Kiislamu kusheherekea siku ya Idd-Ul-Adha.
Waziri wa Usalama wa ndani Dkt Fred Matiangi amechapisha rasmi tangazo hilo katika gazeti la serikali ili kuwawesha wakenya wote kumpumzika siku hiyo.
Kulingana na dini ya Kiislamu, Sikukuu ya Idd-Ul-Adha husheherekewa na Waumini wa dini hiyo kwa kuambatana na mafunzo ya Mwenyezi Mungu kwa kuchinja jinsi Nabii Ibraham alivyotoa sadaka kwa Mungu.
Sherehe za Idd-ul-Adha pia zinatamatisha Hijja ambayo hufanyika kila mwaka katika mji mtakufu wa Macca nchini Saudia Arabia.