Picha kwa hisani –
Wito umetolewa kwa serikali ya kitaifa kuhakikisha wakenya wote wanapata nakala za ripoti ya BBI.
Kulingana na baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta, wanasema ni jambo la kufedhesha kwa wakenya kuambiwa wasome ripoti hio na bado wahusika hawasambaza nakala hizo kwa wananchi mashinani.
Hata hivyo baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta sasa wanapendekeza mchakato wa BBI kusitishwa hadi pale janga la Corona litakapokabiliwa.