Naibu wa Rais nchini William Ruto amesema kuwa Kenya inathamini uhuru wa wanahabari.
Akizungumza jijini Nairobi amesema kuwa serikali itazidi kuulinda uhuru wa wanahabari ili jamii izidi kupata ufahamu wa mambo yalivyo.
Ruto aidha amewatahadharisha wanahabari dhidi ya kuandika habari gushi na badala yake kueneza ukweli kupitia taarifa zao.
“Kenya inatoa nafasi ya uhuru wa wanahabari na kama serikali sisi tuna amini na tumesimamia haki ya wanahabari kuendeleza kazi zao,” amesema Ruto.
Ruto amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Ofisi kubwa za BBC Afrika Mashariki na pembe ya Afrika, hafla iliyofanika jijini Nairobi.
Taarifa na Dominick Mwambui.