Takriban makundi 50 ya wakaazi wa Sabaki eneo la Magarini yanakila sababu ya kutabasamu baada ya kupata mradi wa ng’ombe kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kilifi.
Akiongea wakati wa kupeana Ngombe hizo, afisa mkuu kutoka kwa wizara ya kilimo na ustawi wa mifugo kaunti ya kilifi Fredrick Kaingu amesema kuwa ngombe hizo 50 zimeigharimu serikali ya kaunti ya kilifi shilingi milioni 9 na laki sita.
Afisa huyo amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha kuwa wakaazi wanajitegemea wenyewe kupitia mradi huo wa kuzalisha maziwa ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na changamoto za umaskini katika kaunti ndogo ya Magarini.
Akihudhuria hafla hiyo Mbunge wa Magarini, Michael Kingi pia amesema kuwa mradi huo kwa mara ya kwanza kufika katika eneo hilo utainua hata zaidi maisha ya wakazi.
Taarifa na Charo Banda.