Serikali imetakiwa kuwaangazia watu walio na akili taahira hasa katika kaunti ya Mombasa baada ya takwimu za watu hao kuongezeka kila uchao.
Mwanaharakati wa maswala ya akina mama kutoka Shirika la ‘Mombasa Women Empowerment Network’, Bi Amina Abdallah amesema Serikali imeangazia mipangilio ya virusi vya Corona, huku watu walio na akili taahira wakirandaranda ovyo barabarani.
Akizungumza katika kituo cha kuwatibu watu walio na maradhi ya akili cha Portreitz kule Changamwe, Bi Abdallah amesema tayari ana mipango ya kuwanasa wagonjwa wengine wa maradhi hayo zaidi ya 100 ili watibiwe.
Wakati uo huo, ameitaka Serikali ya kaunti ya Mombasa kuwekeza zaidi katika matibabu kwa watu hao kadri inavyojizatiti kuboresha vitengo tofauti vya kiafya katika kaunti hiyo.