Story by Gabriel Mwaganjoni-
Ni sharti Serikali iweke wazi swala la watu kutiwa nguvuni na kupotezwa au kuuwawa na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa polisi katika Ukanda wa Pwani.
Naibu mkurugenzi wa Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la Haki Afrika Salma Hemed amesema Serikali imejitenga na swala hilo huku ikifahamu wazi kwamba inahusika pakubwa katika utata huo.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Salma amesema ni sharti Serikali ijitokeze waziwazi na kulikomesha swala hilo tata.
Salma amewataka maafisa wa polisi kukomesha maonevu hayo akisema yamewatia uchungu na chuki wakaazi wa Ukanda wa Pwani.