Story by Bakari Ali –
Serikali imehimizwa kuingilia kati na kuwanusuru wakenya wanaopitia masaibu mbalimbali katika mataifa ya mashariki ya kati.
Ismael Kevin Wagidhinji ambae ni mmoja wa walionusurika na masaibu hayo kutoka taifa la Saudi Arabia, amesema amekuwa akizuiliwa katika gereza la taifa hilo kinyume na sheria za kimataifa za wafanyakazi.
Wagithinji amedokeza kuwa zaidi ya wakenya 100 wanaendelea kuzuiliwa katika geraza hilo huku ubalozi wa Kenya nchini humo ukipuuza vilio vya wakenya hao.
Kwa upande wake, Nargis Khamis mama wa mkenya mmoja anayezuliwa nchini humo ameitaka serikali kuingilia kati swala hilo na kuwasaidia wakenya hao wanaopitia hali ngumu nchini humo kurudishwa nchini Kenya.
Akizungumzia swala hilo, Naibu mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika Salma Hemed ameitaka serikali kutoa suluhu mwafaka kwa masaibu yanayowakumba wakenya katika taifa hilo.