
Mkurugenzi wa shirika la Reach Out Centre Trust, Taib Abdulrahman.
Taarifa na Mwahoka Mtsumi
Mombasa, Kenya, Juni 26 – Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na ulanguzi haramu, wadau mbalimbali wamejitokeza na kuwarai vijana kutokubali kushawishi vibaya na kujitosa katika na jinamizi hilo.
Shirika la kupambana na utumizi wa dawa za kulevya Pwani la ‘Reachout Centre Trust’ kupitia Mkurugenzi wake mkuu Taib Abdulrahman, swala la utumizi wa mihadarati pwani limekithiri mno na linahitaj kukabiliwa.
Taib ameitaka serikali kuibuka na mikakati mwafaka itakayohakikisha walanguzi wakuu wa dawa za kulevya wanatiwa nguvuni na wala sio kuwahangaisha watu waraibu kwani wahaitaji tiba.
Kwa upande wake Shirika la kupambana na mihadarati na vileo haramu nchini NADACA, limeitaja jamii kujitokeza waziwazi na kuunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya nchini hasa katika ukanda wa Pwani.