Taarifa na Sammy Kamande.
Jamii ya watu wanaoishi na Ulemavu katika kaunti ya Mombasa, sasa inaitaka serikali ya kitaifa kuwaajiri watafsiri wa lugha ishara ili wajumuike na maafisa wa kuhesabu watu wakati wa zoezi la sensa.
Katibu wa Shirika la Walemavu mjini Mombasa Ruth Awinja amesema walemavu ambao hawana uwezo wa kuongea hawataweza kupeana idadi kamili ya watu wa familia yao hali ambayo itachangia kupata idadi duni.
Awinja ameitaka serikali kuangazia suala hilo kwa haraka kabla ya shughuli hiyo kuanza rasmi hapo kesho.
Wakati uo huo amewataka wazazi kutowaficha watoto wao wenye ulemavu wakati wa zoezi hilo ili kuhakikisha serikali inapata idadi kamili.