Ni sharti Serikali itilie mkazo swala la taasisi za kiufundi ili ikabiliane kikamilifu na uhaba wa ajira nchini.
Afisa anayesimamia mradi wa kuwajenga uwezo vijana unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza Benson Macharia amesema hakuna hatua zozote zitakazoafikiwa kimaendeleo iwapo vijana wataachwa nyuma.
Akiwahutubia jumla ya Wanafunzi 350 waliofuzu katika taaluma mbalimbali za kiufundi katika hafla iliyoandaliwa katika ‘Uwanja wa mbuzi’ kule Kongowea kaunti ya Mombasa, Macharia amesema iwapo Serikali itaekeza katika taasisi za kiufundi basi vijana wengi watasaidika.
Aidha amehoji kuwa mradi huo kufikia sasa umewanufaisha zaidi ya vijana 2,500 katika kaunti zote sita za Pwani na unalenga kuwafikia vijana wengi zaidi.
Taarifa Gabriel Mwaganjoni.