Swala la uhaba wa Walimu lingali changamoto kuu katika sekta ya elimu nchini, na Serikali imetakiwa kuliangazia ili kuimarisha viwango vya elimu nchini.
Mbunge wa Jomvu Badi Twalib ametaja ongezeko mara dufu la Wanafunzi katika shule za upili na msingi kama linalohitaji idadi ya kutosha ya Walimu, akilitaka swala hilo kuangaziwa kama la dharura.
Akizungumza katika eneo bunge lake la Jomvu, Badi amesema sekta ya elimu kamwe haiwezi kuendelezwa kiholela huku Serikali ikifahamu bayana elimu ya msingi bila malipo imeleta mabadiliko makubwa katika shule za msingi kwa kuongeza mara dufu idadi ya Wanafunzi.
Badi amezindua vikao vya kuzijadili changamoto zinazoikumba sekta ya elimu katika eneo bunge lake la Jomvu, huku uhaba wa Walimu, umaskini, utepetevu miongoni mwa Wazazi changamoto za kimiundo msingi vikitajwa kama vikwazo katika sekta hiyo.