Mshirikishi mkuu wa shirika la kijamii la ONUG tawi la Mombasa Zakiah Mohamed amelitaka jopo kazi lililobuniwa kufuatilia na kuendeleza maridhiano kati ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga kuwajumuisha vijana ili kufanikisha uwiano wa taifa.
Akizungumza mjini Mombasa Zakiah amelishinikiza jopo kazi hilo kuwajumuisha vijana kikamilifu ili watoe maoni yao kuhusiana na harakati za kujenga uwiano wa taifa hili.
Kulingana na Zakiah vijana wana mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa na ni muhimu wahusishwe katika hatakati za kufanikisha ustawi wa taifa ikizingatiwa kuwa idadi kubwa ya watu nchini ni vijana.
Kauli yake inajiri huku jopo kazi hilo linaloongozwa na wakili Paul Mwangi likiendelea kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo yao ya kufanikisha uiano wa taifa.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.