Serikali imetakiwa kushirikiana na jamii katika kupambana na mihadarati pamoja na visa vya utovu wa usalama ambao unaendelewa kushuhudiwa katika maeneo mbali mbali Mombasa.
Kulingana na mkurugenzi wa shirika la kupambana na uraibu na dawa za kulevya la Reach Out Trust, Taib Abdulrahman, mgawanyiko baina ya serikali, vijana na jamii umechagia utovu wa usalama.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa baraza la maimamu na wahubiri wa humu nchini Mohammed Khalif amewataka wakaazi kuishi kwa amani na kusherehekea sikukuu ya Eid bila ya fujo lolote.