Story by Hussein Mdune-
Wadau wa maswala ya elimu kaunti ya Kwale wamesema sekta ya elimu nchini itaimarika zaidi iwapo Wizara ya elimu nchini itashirikiana na wadau hao hadi mashinani.
Wadau hao wakiongozwa na Hamisi Rai Nyondo wamesema kuna haja ya idara zingine za kiserikali kushirikiana ili wanafunzi wasaidike zaidi kimasomo na kuboresha viwango vya elimu kanda ya Pwani.
Hamis ambaye pia ni Mkurugenzi wa shule ya kibinafsi ya Muungano amesema endapo sekta zengine zitashirikiana na wadau wa elimu basi visa vya dhulma dhidi ya watoto vitapungua kaunti ya Kwale.
Wakati huo huo amewataka wazazi kuwajibikia majukumu yao ya ulezi wakati huo ambapo watoto wako nyumbani kwa likizo ndefu ya mwezi Disemba.