Story by Janet Shume-
Wanawake wanaoendeleza shughuli za uhifadhi wa mazingira katika fuo ya bahari hindi ya Munje eneo bunge la Msambweni, wameihimiza serikali ya kaunti kuwatambua ili kuwapiga jeki katika shughuli zao.
Wakiongozwa na Yususf Baishe, wamesema licha ya wanawake wengi katika eneo hilo kujitolea kuhifadhi mazingira hususan baharini ikiwemo kupitia upanzi wa mikoko, wengi wao hawajapata elimu ya kutosha kuendeleza shughuli hizo.
Baishe amesema iwapo juhudi zao zitaungwa mkono basi mikakati ya kuhifadhi mazingira itaendelezwa na kila mkaazi katika jamii.
Wakati uo huo, wanamazingira hao wamesihi wadau mbalimbali wa kimazingira kutoa ufadhili kwa wanawake hao ili kuwawezesha kuendeleza uhifadhi wa mazingira bila changamoto.