Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Pwani Profesa Halimu Shauri amesema ajenda nne kuu za serikali zitafaulu kwa kiwango kikubwa endapo serikali itakabiliana vilivyo na swala la ukosefu wa usalama nchini.
Akihutubu kwenye Sherehe ya kuadhinisha siku ya kutozua fujo katika jamii, Profesa Shauri amehoji kuwa kaunti nyingi humu nchini hususan za ukanda wa Pwani zingali bado zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa usalama.
Shauri ameihimiza serikali kuorodhesha ajenda ya usalama kama ilivyoorodhesha ajenda zingeni ili kuhakikisha taifa linaimarika kiuchumi.
Kwa upande wake, Afisa wa maswala ya jinsia na haki za watoto katika Shirika la MUHURI, Topista Juma amesema kuna haja ya serikali kubuni mbinu mbadala za kupambana na ukosefu wa usalama humu nchini.
Taarifa na Hussein Mdune.