Serikali imetakiwa kuifanyia mabadiliko sheria ya polisi ya mwaka wa 2011 kabla ya kutekeleza mageuzi katika Idara ya polisi nchini.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika linaloangazia maswala ya amani na usalama hapa Pwani la Kenya Community Support Centre Bi Phyllis Muema amesema kwamba Serikali inaharakisha mfumo wa mageuzi katika idara ya usalama hali itakayozua utata mwingi badala ya kuimarisha usalama mashinani.
Akizungumza huko Kisimani katika Kaunti ya Mombasa hii leo, Bi Muema anaitaka Serikali kukoma kuiga mifumo ya kiusalama ya mataifa ya nje na badala yake kujadiliana na wadau mbalimbali na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuhusu jinsi mabadiliko hayo yangefaa kutekelezwa mashinani.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.