Mwanasiasa wa chama cha Jubilee kutoka kaunti ya Mombasa Abdi Daib ameitaka serikali kuu kujitenga na shinikizo zinazotolewa na baadhi ya viongozi za kuondoa maafisa wa KDF nchini Somalia.
Kulingana na Daib iwapo serikali itaondoa vikosi vya ulinzi vinavyoshika doria nchini Somali huenda visa vya mashambuliza ya kigaidi humu nchini vikaongezeka.
Hata hivyo amewataka vijana wa humu nchini kutokubali kutumiwa vibaya na makundi ya kigaidi kuvuruga usalama wa taifa hili.
Wakati uo huo ameitaka idara ya usalama kuibuka na mbinu zitazowakinga vijana dhidi ya kujiunga na makundi ya kigaidi ili kuhakikisha usalama wa taifa unadhibitiwa.
Taarifa na Hussein Mdune.