Ili kuhakikisha kuendelea kwa shughuli za Serikali bila shida yeyote na kutimizwa kwa majukumu katika Hazina ya Kitaifa na Wizara husika kufuatia agizo la Mahakama linalomhusu Waziri wa Hazina ya Kitaifa na Mipango Bw. Henry Rotich na Katibu wa Hazina ya Kitaifa Dkt. Kamau Thugge, Rais amefanya mabadiliko yafuatayo Serikalini:
(I) Mheshimiwa Balozi, Ukur Yatani Kanacho, ambaye ni Waziri wa Masuala ya Wafanyakazi na ya Kijamii, pia atakuwa kaimu Waziri wa Hazina ya Kitaifa na Mipango
(II) Dkt. Julius Monzi Muia ameteuliwa kuwa Katibu katika Wizara ya Hazina ya Kitaifa.
(III) Bw. Torome Saitoti ameteuliwa kuwa Katibu katika Idara ya Mipango.
(IV) Meja Mstaafu Jenerali Gordon Kihalangwa ameteuliwa kuwa Katibu katika Wizara ya Ulinzi.
Good job…twagitaji kazi ifanyike sasa
Good