Story by Ephie Harusi-
Katibu mkuu msimamizi katika Wizara ya habari, teknolojia na mawasilisiano nchini Eric Kiraithe amesema serikali imeweka mikakati ya kupambana uwizi mitandaoni ambao umekuwa ukitekelezwa.
Kiraithe amesema mpango huo utadhibiti visa vya wananchi kulaghaiwa mitandaoni kwani idadi kubwa ya wakenya wamekuwa wakipoteza fedha nyingi kutipitia mitandao.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Kilifi, Kiraithe amesema mikakati hiyo itachangia kila kituo cha usalama nchini kuwa na afisa aliye na utaalam wa kupambana na uwizi mitandaoni.
Wakati uo huo amewatahadharisha wananchi dhidi ya kufungua faili au vitu wa sivyo vifahamu vinapotumwa mitandaoni, akisema faili hizo huenda zinakawa na ushawishi wa kutoa taarifa za binafsi kwa walaghai.