Katibu katika Wizara ya Utalii na wanyamapori nchini Safina Kwekwe, amesema serikali imeweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha inafufua sekta ya utalii nchini baada ya kusambaratika kufuatia janga la Corona.
Safina amesema licha ya sekta hiyo kutegemewa na wengi ikiwemo kuajiri zaidi ya wakenya milioni 1.6 bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto.
Akizungumza na Wanahabari mjini Kwale, Safina amesema juhuzi zaidi zitaekezwa ili kuhakikisha sekta ya Utalii nchini inaboreshwa zaidi.
Wakati uo huo amesema licha ya idadi ya watalii wanaozuru nchini kupungua kutokana na masharti ya kudhibiti maambukizi ya Corona, Wizara hiyo itafanya kila juhudu kuhakikisha inaboresha vivutio vya utalii nchini.