Picha Kwa Hisani
Waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe ameagiza wananchi kuanza tena kuvaa barakoa katika maeneo ya umma, sawa kuzingatia masharti mengine ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona ili kudhibiti wimbi jengine la maambukizi.
Kagwe vile vile amesema lazima wananchi wavae barako wanapokua katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo kwenye magari ya uchukuzi wa umma ,kwenye ndege, ofisini ,katika maduka ya jumla na katika nyumba za ibada.
Kagwe amesema maambukizi ya corona yameonekana kuongezeka msimu huu wa baridi hali ambayo inaipa hofu wizara ya afya nchini na kwamba lazima wananchi waanze tena kuzingatia masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.
Kagwe hata hivyo amesema wakati huu ambapo maambukizi ya corona yameanza kupanda, wakenya wanapaswa kuchukua tahadhari zaidi ili kuepuka yalioshuhudiwa mwaka 2020 na mwaka 2021 ambapo watu wengi walipoteza maisha sawa na kupotea kwa rasilimali.
Kagwe aidha amewataka wale ambao hawajapokea chanjo dhidi ya virusi vya corona kujitokeza na kupokea chanjo ili kudhibiti makali ya virusi vya Corona.