Story by Mwahoka Mtsumi –
Wakili na mchanganuzi wa maswala ya kisheria George Kithi amesema kutothaminiwa kwa mimea ya Pwani kama vile Mkorosho na Mnazi kumetokana na viongozi wa siasa kutotunga sheria za kuiwezesha mimea hiyo kuwanufaisha wakaazi.
Wakili Kithi amesema kutokana na hali hiyo kumechangia mimea hiyo ambayo ndio tegemea kuu la mkaazi wa Pwani katika kujiimarisha kiuchumi kukosa kutambuliwa na serikali ya kitaifa.
Wakili Kithi amesema ndani ya miaka 60 ya uhuru wa taifa hili mimea ya Pwani haijawanufaisha vilivyo wenyeji kinyume na mimea inayokuzwa katika maeneo mengine ya nchini kama vile Mkahawa na Majani chai.
Wakati uo huo ameelezea masikitiko yake kutokana na jinsi ambavyo wakaazi wa Pwani wangali wanahangaishwa na maafisa wa usalama katika biashara zao za uuzaji wa pombe ya mnazi.
Hata hivyo ameahidi kuishinikiza serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha inaibuka na sheria muafaka itakayohakikisha serikali inauthamini mmea wa Mkorosho na Mnazi.