Picha kwa hisani –
Serikali ya kaunti ya Mombasa imewafuta kazi madaktari 86 na wataalam wengine wa kiafya akiwemo Katibu mkuu wa Chama cha Madaktari nchini KMPDU Dkt Chibanzi Mwachonda kwa kushiriki mgomo.
Tangazo hilo, limetolewa rasmi na serikali ya kaunti ya Mombasa huku Madaktari katika kaunti hiyo wakiapa kutorudi kazini hadi matakwa yao yatakapotimizwa.
Katibu wa Chama cha Madaktari nchini KMPDU tawi la kaunti ya Mombasa Daktari Abidan Mwachi, amesema Madaktari hao hawatarudi kazini hadi pale Serkali ya kaunti hiyo itakapowalipa mishahara yao.
Kulingana na Daktari Mwachi, Serikali ya kaunti ya Mombasa imewapuuza na kudinda kufanya mazungumzo na madaktari hao ili kuusuluhisha mgomo huo sawia na kuwapa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Corona.
Wakati uo huo ameitaka Serikali ya kaunti hiyo kukoma kuwatisha madaktari hao na badala yake kuwatendea haki.