Picha kwa hisani –
Serikali ya kaunti ya kilifi kupitia kwa wizara ya afya kaunti hiyo, imesema imeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na masuala ya dharura ikiwemo ajali za barabarani, ili kuokoa maisha ya wakaazi.
Charles Dadu Karissa waziri wa afya kaunti hiyo, amesema wametayarisha mafunzo kwa kitengo kinachoshughulikia masuala ya dharura kaunti hiyo, ili kuboresha ujuzi wao wa jinsi ya kushugulikia masuala hayo yanapotokea.
Wakati uo huo Dadu amesema vyumba vya kupokea wagonjwa wanaohitaji matibabu ya kiwango cha juu, vinaendelea kuboreshwa pamoja na kuwekwa vifaa hitajika kwa ajili ya matibabu.
Huku wauguzi watakaoshughulikia vyumba hivyo, wakiwa wamepokea mafunzo mbadala ya jinsi ya kutoa huduma za matibabu kwa njia ipasayo, ili kuhakikisha wagonjwa wanapokea huduma bora za afya.