Story by Gabriel Mwaganjoni –
Serikali ya kaunti ya Taita taveta imewahakikishia wakaazi wa kaunti hiyo kwamba hospitali na zahanati zote za umma zina dawa za kutosha.
Waziri wa afya katika serikali ya kaunti hiyo John Mwakima amesema Serikali ya kaunti ya Taita taveta imelipa kipau mbele swala la afya huku akiwataka wakaazi kutokuwa na hofu yoyote.
Akizungumza alipozuru katika hospitali kuu ya rufaa ya Moi mjini Voi, Mwakima amesema huduma za afya katika kaunti hiyo zitaboreshwa zaidi ili wakaazi wa wapate huduma bora.
Kulingana na Mwakima, japo Serikali ya kaunti hiyo imekuwa ikidaiwa na Mamlaka ya kusambaza dawa nchini KEMSA, imejizatiti kulipa polepole madeni hayo na Shirika hilo halijakatiza usambazaji wa dawa katika kaunti hiyo.