Story by Gabriel Mwaganjoni-
Serikali ya kaunti ya Mombasa imetakiwa kuwekeza angalau shilingi milioni 100 kwa kila eneo bunge la kaunti hiyo ili kuwakimu vijana kwa elimu ya juu zaidi.
Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amesema japo vijana wana ari ya kujiendeleza kimasomo, wengi wao wamekosa uwezo wa karo.
Akizungumza katika eneo bunge la Changamwe, Mwinyi amesema wavulana wamelegeza kamba katika swala la kusaka elimu ya juu sababu kuu ya wao kupotoka na kujitosa katika uraibu wa mihadarati na uhalifu.
Wakati uo huo amesisitiza umuhimu wa vijana kuwa wabunifu na kujiajiri wenyewe.