Picha kwa Hisani –
Serikali ya kaunti ya Mombasa itaupanua mradi wa kuwakimu vijana wa kaunti hiyo kwa ujuzi wa taaluma mbalimbali ili wajikimu kimaisha.
Naibu Gavana wa kaunti hiyo William Kingi amesema kaunti hiyo imekuwa ikitekeleza mradi huo ili kuwanufaisha vijana ambao tayari wameanza kuidhinisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Kulingana na Kingi, vijana wanahitaji elimu ya kiufundi na kuhimizwa kukumbatia suala la kujibunia ajira badala ya kuhangaika wakisaka ajira.
Kingi amesema Serikali ya Kaunti hiyo kwa sasa inaainishia sera maalum iliyotoka kwa vijana wa Kaunti hiyo ili ianze kutekelezwa na kuyaangazia kwa kina maslahi ya Vijana.