Serikali ya kaunti ya Kwale kwa ushirikiana na serikali ya kitaifa inalenga kuiboresha hifadhi ya wanyama pori ya shimba hills ili kuvutia zaidi watalii.
Waziri wa utalii kaunti ya Kwale Ramadhan Bungale amesema kuwa tayari jopo maalum limeundwa litakalo hakikisha mpango huo unaafikiwa.
Bungale aidha ameeleza haja ya wakaazi wa kaunti ya Kwale kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa kuewepo kwa maeneo tengefu ya viumbe vya baharini.
Taarifa na Salim Mwakazi.