Waziri wa ugatuzi na mipango maalum katika serikali ya kaunti ya Kilifi Bi.Rachael Musyoki amehimiza ufuatiliaji wa sheria za ujenzi ili kuzuia majanga ya majengo kuporomoka.
Bi Musyoki amedai kuwa kuna baadhi ya wakaazi ambao wanapuuza sheria za ujenzi wanapojenga majengo yao mbali mbali hatua anayosema imepelekea baadhi ya majengo kuanguka na kusababisha hatari.
Waziri huyo amesema serikali ya kaunti ya Kilifi itaanza kuchunguzwa majengo yote ili kuhakikisha yamezingatia sheria za ujenzi na kuwchukulia hatua za dharura wakaazi ambao wamekiuka sheria hizo kwenye majengo yao.
Kauli ya waziri Musyoki inajiri takriban Juma moja baada ya mkasa wa kuporomoka kwa jumba la ghorofa 8 mjini Malindi na kusababisha maafa ya mtu mmoja na kujeruhiwa kwa wengine 23.
Taarifa na Esther Samini.