Serikali ya kaunti ya Kilifi imehimizwa kulithmini soko la zao la Mnazi ili kuhakikisha wakulima wa zao hilo wananufaika na kuimarisha uchumi wa kaunti hiyo.
Kulingana na Mwanzilishi wa Shirika la ‘Fagio zetu Mali Zetu’, Daniel Yaa Kaingu, kuna haja ya serikali ya kaunti hiyo kulithmini zao la Mnazi na kushirikiana na wakulima kikamilifu.
Yaa anasema tayari wameanzisha Soko la Fagio katika eneo la Kaloleni na wako tayari kushirikiana na viongozi wa kaunti ili kuzuru mashinani na kuwasaidia wakaazi wa kaunti hiyo kimaendeleo.
Kwa upande wake Hildah Mwawashe, amewashauri Akina mama wanzake kujitokeza na kulithmini soko la zao la Mnazi ili kuwasaidia katika kuzikabili changamoto mbalimbali katika familia zao.
Taarifa na Mercy Tumaini.