Picha kwa hisani ya Swahilpot Hub
Mbunge mteule anayewakilisha walemavu katika bunge la kitaifa David Ole Sankok ameitaka Serikali na Mashirika mengine ya kibinafsi kutowabagua watu wanaokumbwa na changamoto za kimaumbile.
Akizungumza katika kituo cha Swahilipot Hub kaunti ya Mombasa wakati wa maadhimisha ya siku ya watu wenye ulemavu wa kusikia, Sankok amesema japo walemavu wanakumbwa na vikwazo kuna majukumu wanayoweza kuyatekeleza ipasavyo.
Sankok ametaka jamii ya walemavu itambuliwe kikamilifu katika ajira, elimu, uongozi miongoni mwa maswala mengine msingi ya kulijenga taifa.
Wakati uo huo, amewataka wazazi kuwapa nafasi watoto walemavu katika maswala mbalimbali na kukomesha ubaguzi.