Serikali ya kitaifa imehimizwa kujitokeza na kuwafadhili waraibu waliokatika tiba ya kujinasua pwani, kwa lengo la kufanikisha jitihada zinazoendelezwa na wanaharakati za kuwanasua vijana kwenye janga hilo.
Afisa mkuu anayesimamia kitengo cha tiba na ushauri kwa watumizi wa dawa za kulevya katika kituo cha MEWA Abdallah Badrus, amesema japo waraibu wengi wana hamu ya kujinasua, wengine wameshindwa kumudu gharama ya tiba hiyo katika vituo vya kibinafsi.
Badrus amesema ni vyema iwapo serikali kuu itashirikiana na mashirika yanayopambana na uraibu huo hapa pwani ili kuwasajili watumizi wa dawa za kulevya katika tiba hiyo kwa lengo la kuwanasua.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni