Story by Janet Shume –
Serikali kuu na ile ya kaunti ya Kwale zimelaumiwa kwa kutoangazia swaala la elimu katika shule za wanafunzi wanaoishi na ulemavu.
Mwalimu mkuu wa shule ya walemavu wa kutoskia mjini Kwale Irene Kimanthi amesema serikali ya kaunti ya Kwale imekuwa ikielekeza misaada mbalimbali kwa shule za kawaida pasi na kujali uhitaji wa wanafunzi katika shule za wanafunzi walemavu.
Irene amesema wanafunzi katika shule za walemavu wamekosa kupata haki zao za msingi ikiwemo kupokea fedha za basari kutoka kwa serikali kuu ama zile za kaunti hali ambayo imechangia wanafunzi wengi ambao wanaishi na ulemavu kusalia majumbani kwa kukosa karo.
Hata hivyo jamii pamoja na wazazi wenye watoto wanaokabiliwa na changamoto za maumbile wamelaumiwa pakubwa kwa kuwatenga watoto wao wenye ulemavu na kuelekeza juhudi zao za ulezi kwa watoto wengine.