Serikali imeweka wazi kuwa itaendelea kuongeza mgao wa fedha kwa serikali za kaunti kila mwaka ili kuhakikisha wananchi wananufaika moja kwa moja.
Waziri wa ugatuzi nchini Eugine Wamalwa amesema tayari mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto zinazozikabili serikali za ugatuzi kutokana na uhaba wa fedha zinakabiliwa.
Amesema japo changamoto iliyopo kwa sasa ni pesa za kaunti kukosa kutumika katika miradi ya maendeleo, lakini ana imani kwamba mikakati iliyoidhinishwa sasa itaimarisha masuala mbalimbali.
Waziri huyo wa Ugatuzi hata hivyo amewaonya viongozi wa kaunti dhidi ya madai ya kutumia fedha kwa miradi ya maendeleo ilhali miradi hiyo haipo, akisema serikali itawakabili kikamilifu kwa mujibu wa sheria.
Taarifa na Mwahoka Mtsumi.