Story by Mwahoka Mtsumi –
Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amesema huenda wakenya wakatumia aina mbalimbali ya chanjo ya Corona kama hatua moja wapo ya kuzuia msambao wa virusi hivyo hatari.
Waziri Kagwe amesema Serikali inatarajia kupokea chanjo ya Johnson na Johnson na ile ya Pfizer kutoka taifa la Marekani ifikapo mwezi Agosti mwaka huu ili kuhakikisha wakenya wote wanapata chanjo.
Katika kikao na Wanahabari, Waziri Kagwe amesema serikali imetenga fedha za kutosha ili kuhakikisha dozi milioni 10 ya chanjo ya Johnson na Johnson inawasili nchini mwaka.
Akigusia swala la magavana kupewa idhini ya kuagiza chanjo ya Corona, Waziri Kagwe amesema swala hilo linatekelezwa na serikali ya kitaifa pekee kwani ndio iliyo na idhini ya kuagiza chanjo kwa kuzingatia njia tatu pekee za kimataifa.