Serikali imetangaza kutoa takribani shilingi milioni 60 kuanzia wiki ijayo kuwafidia zaidi ya waathiriwa 700 waliathiriwa na wanyama pori katika kaunti ya Taita Taveta.
Naibu wa Rais William Ruto amesema serikali pia itatumia shilingi milioni 265 kukamilisha ujenzi wa kilomita 96 za ua wa stima kati ya Kamtonga na Kasighau ili kuzuia wanyamapori kutangamana na binadamu na kusababisha harasa.
Akizungumza mjini Voi katika kaunti hiyo ya Taita Taveta, Ruto amesema ripoti zinaonyesha kuwa visa 10 vya mauaji vilivyochangiwa na wanyamapori katika kaunti hiyo viliripotiwa
Ruto amezindua kituo kipya cha CT Scan katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi, kilichoigharimu serikali shilingi milioni 100 ambapo kitatoa huduma za picha kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakisafiri hadi Mombasa na Nairobi kupata huduma hiyo.
Taarifa na Fatuma Rashid.