Story by Ali Chete –
Waziri wa uchukuzi na miundo msingi nchini James Macharia amewakikishia wakenya kwamba miradi iliyozinduliwa na serikali ya Jubilee chini ya uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta itakamilika kabla ya hatamu ya serikali hiyo kung’atuka mamlakani.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Mombasa, Macharia amesema miradi yote ya serikali inayoendelea kwa sasa katika ukanda wa pwani itakamilika kwa wakati.
Macharia amesema serikali imeweka pesa za kutosha katika miradi tofauti huku akiweka wazi kwamba mradi wa barabara ya Mombasa hadi Jomvu itagharimu bilioni 8.5 na itakamilika mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Kwa upande wake Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang`i ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maendeleo amesema changamoto zinazoikumba miradi hiyo imepekea kusitishwa kwa baadhi ya miradi inayolenga kuwanufaisha wananchi.