Serikali ya kitaifa ikishirikiana na mataifa takriban 13 barani Afrika sasa wameanzisha mchakato wa kuzitambua na kuzihifadhi torati zote na raslimali ambazo zinapatikana chini ya maji ya bahari hindi.
Akiongea na wadau hao ama washirikishi kutoka mataifa mbali mbali huko Malindi kaunti ya Kilifi naibu waziri wa michezo , utamaduni na utalii nchini Hassan Noor amesema kuwa Kenya hasa eneo la Pwani Kuna takriban kilomita 600 ya ufuo wa bahari ambao una raslimali zilizoko chini ya maji ambazo zinafaa kuhifadhiwa.
Aidha waziri huyo msaidizi amesema kuwa hivi karibuni kama mataifa wataanzisha mafunzo mbali mbali katika vyuo vikuu ili kuhakikisha kuwa wadau mbali mbali wanapata mafunzo ya kuhifadhi torati hizo za kihistoria barani Afrika.
Kauli ya waziri huyo imeungwa mkono na waziri msaidizi kutoka nchini Tanzania John Kanyasi ambaye amesema kuwa kuhifadhiwa kwa torati hizo ambazo zinapatikana chini ya maji ya bahari hindi vile vile zitachangia pakubwa ongezeko la mapato ya kitaifa kupitia utalii.
Taarifa na Charo Band.