Story by ALi Chete –
Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu ardhi imeweka wazi kwamba hivi karibu serikali ya kitaifa itagawanya zaidi ya hati miliki elfu 50 za ardhi kwa wamiliki wa ardhi katika maeneo mbali mbali ya ukanda wa pwani.
Kulingana na mbunge wa Ganze Teddy Mwambire ambaye pia ni mwanachama wa kamati hio, zoezi hilo la ugavi wa hati miliki za ardhi litaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Mwambire ameutaja mpango huo wa ugavi wa hati miliki kama utakaosaidia kupunguza mizozo ya mashamba inayoshuhudiwa kila uchao katika kaunti mbali mbali za hapa pwani.
Mwambire amewaonya wakaazi wa ukanda wa pwani dhidi ya kuuza ardhi hizo pindi wanapokabidhiwa hatimiliki , akiwasi wakaazi kuzihifathi vyema stabadhi hizo muhimu ili kumaliza tatizo la Uskwota.
Kauli yake imejiri wakati ulimwengu unaadhibisha siku ya masorovea duniani.