Picha kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amewahakikishia Wakenya kwamba serikali yake itaendelea kuekeza katika mipango inayoboresha maslahi ya vijana nchini.
Rais amesema idadi ya vijana nchini ndiyo raslimali kuu zaidi ya taifa hili, ikiwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuimarisha uchumi wa taifa hili.
Rais Kenyatta amesema vijana wanajumuisha robo tatu ya idadi ya watu nchini, akiongeza kwamba Serikali imeongeza uekezaji wa raslimali katika sekta zinazoshughulikia masuala ya vijana ikiwemo elimu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na uanabishara.
Kiongozi wa Taifa amesema haya katika Ikulu ya Nairobi hapo jana alipoongoza uzinduzi wa mpango wa umoja wa mataifa kwa vijana wa Generation Unlimited (GenU) hapa nchini.