Picha kwa hisani –
Serikali itaboresha mazingira ya kituo cha kiteknolojia na sanaa cha ‘Swahilipot-Hub kaunti ya Mombasa ili kuwawezesha watu walio na ulemavu kuendeleza shughuli zao katika kituo hicho.
Afisa mkuu mtendaji wa bodi ya filamu nchini Dakta Ezekiel Mutua amesema kituo hicho kina umuhimu mkubwa katika sanaa na teknolojia nchini hivyo basi kinapaswa kuboreshwa.
Akizunguzma alipozuru katika kituo hicho, Mutua amesema vijana walemavu walio na talanta wamekabiliwa na changamoto katika kuendeleza shughuli zao kituoni humo.
Wakati uo huo, amesema kituo hicho kitapokea ufadhili wa vifaa mbalimbali vya kuwasaidai vijana kujiendelea katika talanta zao.