Story by Mwanaamina Fakii-
Serikali ya kitaifa inalenga kuanzisha zoezi la ugavi wa chakula cha msaada kwa wakaazi walioathirika na baa la njaa katika maeneo ya Kinango, Matuga na Lungalunga.
Kamishna wa kaunti ya Kwale, Gideon Oyagi amesema zoezi hilo litaanza rasmi siku ya Jumatano kwani zaidi ya familia takriban elfu 100 zinahitaji msaada wa chakula na maji katika maeneo hayo.
Oyagi amesema Shirika la Chakula Duniani FAO pamoja na shirika la msalaba mwekundu yana mpango wa kupeana pesa kwa familia hizo ambazo zimeathirika na ukame ili kujikimu kimaisha.
Wakati uo huo amedokeza kwamba maafisa wa serikali bado wanaendelea utathmini wa kina katika maeneo ambayo familia takriban elfu 100 zimeathirika pakubwa na ukame ili kuhakikisha msaada huo wa chakula unawafikia wakaazi hao.