Story by Rasi Mangale –
Serikali kuu inaendeleza mikakati ya uchimbaji mabwawa madogo 300 katika maeneo kame nchini ili kukabiliana na uhaba wa maji katika maeneo hayo.
Katibu katika Wizara ya Kilimo Prof Hamadi Boga amesema kuchimbwa kwa mabwawa hayo kutahakikisha wananchi wa maeneo kame pamoja na mifugo wao hawataabiki wakati wa kiangazi.
Prof Boga amehoji kuwa kuchimbwa kwa mabwawa makubwa katika kaunti ya Kwale ikiwemo bwawa la Mwache kutasuluhisha tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji.