Story by Our Correspondents –
Waziri wa Elimu nchini Prof. George Magoha ametangaza kwamba serikali tayari imetoa shilingi bilioni 17.5 kwa shule za msingi na upili kufadhili masomo ya muhula wa pili.
Waziri Magoha amesema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 15.5 zitasambazwa kwa shule za upili kote nchini huku shilingi bilioni 22 zikisambazwa kwa shule za msingi ili kuhakikisha shughuli za masomo zinaendeshwa vyema.
Waziri Magoha amedokeza kuwa kama Wizara wameweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha shughuli za masomo zinaendeshwa bila ya changamoto zozote huku akiahidi kwamba serikali itafanya kila juhudi kuhakikisha wanafunzi wanafanya vyema shuleni.
Hata hivyo shule zote kote nchini zinatarajiwa kufunguliwa rasmi Oktaba 12 wiki ijayo kwa muhula wa pili.