Story by Gabriel Mwaganjoni –
Serikali imeteketeza jumla ya magunia 800 ya Sukari yenye thamani ya shilingi milioni 4 katika eneo la Kibarani kaunti ya Mombasa.
Mshirikishi wa Utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema hatua hiyo inakamilisha msako wa bidhaa ghushi ambao umekuwa ukitekelezwa na vitengo mbalimbali nchini.
Elungata amesema msako huo utaendelezwa mara kwa mara ili kulisafisha soko la Pwani lililosheheni bidhaa bandia.
Afisa huyo tawala amewataka Wafanyibiashara wa Pwani kuzingatia masharti yote na kutoingiza bidhaa ghushi nchini zinazohatarisha maisha ya wananchi.