Story by our Correspondents –
Serikali imetangaza marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi kwa mda wa siku 30 katika maeneo ya Mpeketoni, Mkunumbi, Witu na Hindi katika kaunti ya Lamu.
Katika tangazo lililotolewa na Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i, serikali imechukua hatua hiyo baada ya kushuhudiwa kwa shambilizi ya kivamizi katika kijiji cha Widhu eneo la Majembeni kaunti ya Lamu hali ambayo ilisababisha watu 7 kuaga dunia.
Matiang’i amesema wakati wa masaa ya kafyu katika maeneo hayo maafisa wa usalama watakuwa wakiendeleza oparesheni ya kuwasaka magaidi wanaotekeleza mashambulizi ya kivamizi.
Hata hivyo amedokeza kwamba ni lazima wakaazi wote wa maeneo hayo kuzingatia masaa ya kafyu na yeyote atakayepatikana akirandaranda ovyo wakati wa kafyu atakabiliwa kisheria.