Picha kwa hisani –
Serikali imetakiwa kuitekeleza kikamilifu katiba ili kufanikisha mchakato wa mageuzi nchini.
Mwanaharakati wa kijamii Kanda ya Pwani Bi Phyllis Muema amesema katiba ina vipengele muhimu mno ambavyo iwapo vitatekelezwa kikamilifu, taifa hili litapiga hatua kidemokrasia, kiuongozi na kimaendeleo.
Kulingana na Muema, taasisi zilizoko kwenye katiba zinapaswa kujengwa na kuwezeshwa kuyatekeleza majukumu yake kikamilifu.
Aidha Mwanaharakati huyo wa kijamii ameitaja katiba kama iliyo na manufaa msingi kwa mwananchi mashinani, akiwataka Viongozi wakuu kuithamini na kutekeleza kikamilifu.