Story by Mimuh Mohamed –
Serikali ya kitaifa imepiga marufuku safari za ndege kati ya Kenya na Somalia agizo ambalo limeanza kutekelezwa punde tu baada ya ripoti hiyo kutolewa rasmi kwa umma.
Mamlaka ya kusimamia safari za ndege nchini KCAA ambayo imetangaza rasmi marufuku hiyo haijatoa sababu kamili zilizopelekea kuzuiwa kwa ndege zinazoendeleza safari kati ya Kenya na Somalia kutotoka au kuingia humu nchini.
Marufuku hiyo hata hivyo imeidhinishwa siku chache baada ya Qatar kupatanisha mataifa haya mawili kutokana na mgogoro wa kidiplomasia kati ya Mogadishu na Nairobi.
Kenya imeonekana kuingia kwenye mgogoro na Somalia baada ya taifa hilo kuishutumu Kenya kwa kuingilia masuala yake ya ndani.